The House of Favourite Newspapers

Simba Yamtangaza Mkuu wa Kitengo cha Kusaka Vipaji (Skauti)

0

Klabu ya Simba imemtangaza Mels Daalder kuwa Mkuu wa kitengo cha kusaka vipaji (Skauti) wa klabu hiyo kuelekea dirisha la usajili kwa ajili ya msimu ujao.

Mels raia wa Uholanzi ambaye ana uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali ameshiriki kozi mbalimbali za uskauti duniani ikiwa ni pamoja na kozi zikizoendeshwa na Skauti wa zamani wa Manchester United David Hobson.

Mels ameshawahi kuishi Tanzania, ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na ana ujuzi mkubwa na ufahamu mkubwa wa ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika.

Leave A Reply