The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Uso kwa Uso na Zitto, Rungwe & Lipumba

0

Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Desemba 15, 2021 amefungua mkutano wa wadau wa vyama vya siasa nchini ambao unalenga kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini unaofanyika jijini Dodoma.

 

Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika jijini Dodoma umeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Baraza la Vyama vya Siasa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na wenyeviti wa vyama kadhaa akiwemo Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Augustino Mrema (TLP), Hashim Rungwe (Chauma) na John Shibuba (ADA-TADEA).

 

Wengine ni John Cheyo (UDP), Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, Mwenyekiti wa ADC, Hamad Rashid Mohamed, wenyeviti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa na Zanzibar, Jeshi la Polisi, Spika Mstaafu Anne Makinda, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba na wengineo.

 

Vyama viwili vya Chadema na NCCR-Mageuzi havikuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya kile walichodai ni kukosekana kwa utashi wa kisiasa na uhuru na kuzuiwa mikutano ya kisiasa.

 

Leave A Reply