The House of Favourite Newspapers

Zitto Amuomba Rais Samia Amsamehe Mbowe -Video

0

Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe amemuomba Rais Samia kuwasaidia kumtoa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ili waungane naye katika kujenga taifa.

Zitto ameyasema hayo alipopata nafasi ya kuongea kwenye Mkutano wa Wadau wa Kujadili Hali ya Demokrasia ya Vyama Vingi Nchini uliofanyika leo Desemba 15, 2021 katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

 

”Sisi viongozi wa Vyama tupo hapa lakin na kuna mwenzetu hayupo kwasababu ya changamoto za kisheria na tuna utamaduni sisi wa kumaliza haya mambo na haitakuwa mara ya kwanza, tunakuomba sana kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za kisheria tusaidie mwenzetu tuwe naye,” ameeleza Zitto Kabwe.

 

Katika hatua nyingine Zitto ameeleza wanavyouchukulia Mkutano huo. ”Hatua hii sisi tunachukulia kuwa ni muhimu sana kuelekea katika kuwa na majadiliano ya kisiasa katika nchi yetu na kila jambo lina mwanzo na huu ni mwanzo mwema na Mungu atatuongoza tuweze kuwa na utaratibu huu kama ambavyo tulivyo Tanzania”.

Leave A Reply