The House of Favourite Newspapers

Rais wa Barcelona; Messi Anataka Kumalizia Soka Lake hapa

0

RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, amefunguka kuhusu tetesi zinazosambaa juu ya hatima ya supastaa Lionel Messi, akisisitiza kuwa Muargentina huyo atabaki klabuni hapo kwa maisha yake yote ya soka.

 

Tetesi zilisambaa kwa kasi wiki iliyopita zikisema kuwa Messi amegoma kuongeza mkataba mpya Barcelona na ameamua kuondoka mkataba wa sasa utakapomalizika mwakani.

 

Messi bado hajasema chochote hadharani kuhusiana na tetesi hizo, ingawa ukimya wake pekee unatoa tafsiri kwa wengi kwamba huenda hakubaliani na utawala wa Bartomeu.

 

Lakini Bartomeu amesisitiza kuwa anaamini nyota huyo mwenye miaka 33, atasaini mkataba mpya na atamalizia soka lake Barca.”Siwezi kuzungumza kwa undani lakini Messi ameshasema mara nyingi kuwa atamalizia soka lake Barcelona,” alisema.

“Tumejikita kwenye mashindano na kuna mazungumzo na wachezaji wengi. Messi anataka kuendelea na anataka kumalizia soka lake hapa. Ana miaka mingi imebaki na tutamfurahia kwa muda mrefu zaidi.

 

“Messi juzi alionyesha kwa mara nyinginte tena umuhimu wake Barcelona baada ya kutoa asisti mbili wakati Barca ikiichapa Villareal 4-1 ugenini. Muargentina huyo sasa amefikisha asisti 19 za La Liga msimu huu zikiwa ndiyo nyingi zaidi kwake kuwahi kutoa kwa msimu tangu aanze kucheza soka

Leave A Reply