The House of Favourite Newspapers

Rais wa Jamhuri ya Romania, Klaus Iohannis Kufanya Ziara ya Kitaifa nchini

0
Rais wa Jamhuri ya Romania, Klaus Iohannis.

Rais wa Jamhuri ya Romania, Klaus Iohannis, atafanya Ziara ya Kitaifa nchini kuanzia tarehe 16 hadi 19 Novemba 2023 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Lengo la ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Romania pamoja na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kama Uwekezaji, Elimu, Utalii, Afya na Utamaduni.

Uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji Tanzania na Romania zimeendelea kushirikiana katika sekta ya biashara na uwekezaji ambapo bidhaa kuu za Tanzania zinazouzwa Romania ni minofu ya samaki aina ya sangara, chai, tumbaku na parachichi. Tanzania inanunua kutoka Romania bidhaa za mashine za umeme, vifaa vya matrekta, magari na vifaa vya matibabu.

Kupitia ziara hii Tanzania na Romania zimedhamiria kuinua na kuimarisha kiwango cha biashara kati ya nchi hizi mbili ambacho licha ya Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nchini Romania, kiwango cha biashara kati ya Mataifa haya mawili bado ni kidogo na kimeshuka katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na fursa za kibiashara zilizopo.

Leave A Reply