The House of Favourite Newspapers

Makonda: CCM Yaelekeza Pikipiki Zilizokamatwa Silali Zirudishwe Na Kukiwa Na Mali Zitozwe Kodi

0
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda

Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Wananchi wa Tarime Mkoani Mara  Novemba 14, 2023

“Ninafahamu ya kwamba zipo bodaboda zilizotumia fursa ya mpaka kufanya biashara za magendo hilo halipingiki na mimi ni msema ukweli lakini wapo Wananchi ambao wameendelea kufanya shughuli zao katika kusongesha maisha yao na hili sio la kupinga”

“Sasa Maelezo ya CCM na Mkuu wa Mkoa upo hapa Mhe. Mtanda upo hapa, na nimemsikia Mhe. Waitara anasema nimpigie simu Waziri wa Fedha, sasa hili swala wala sio la kupiga simu ni maelekezo tu ya Chama Cha Mapinduzi, kuanzia sasa leo tarehe 14 hadi ifikapo kesho tarehe 15 pikipiki zote zilizokamatwa Silali warudishiwe pikipiki zao na kama kuna mali zilizokamatwa watozwe kodi warudishiwe mali zao na kuanzia hapo utaratibu wa kisheria ufuate mkondo wake, wapeni fursa watu wafanye biashara kama ni bodaboda alipe kodi, ushuru achukue bidhaa auze, CCM Oyeee” amesema Paul Makonda

Leave A Reply