The House of Favourite Newspapers

Rais wa Marekani, Joe Biden Aliomba Bunge Kuidhinisha Msaada wa Silaha

0
Rais wa Marekani, Joe Biden.

Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumatano ameliomba bunge la Marekani, kuidhinisha msaada zaidi wa silaha kwa Ukraine, akisema kushindwa kupitisha msaada huo itakuwa zawadi kubwa ya Marekani, kwa rais wa Russia, Vladimir Putin.

Zawadi hiyo itamuwezesha kushinda vita vya karibu miaka miwili vya rais Putin, dhidi ya nchi hiyo jirani. Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ya Marekani, imetangaza msaada mpya wa usalama kwa Ukraine ambao ni mgao wa 52 wa utawala wa rais Biden wa vifaa kwa ajili ya Ukraine toka Agosti 2021.

Msaada huo unajumuisha mfumo wa ulinzi wa anga, risasi za kivita, silaha za kuzuia mashambulizi ya vifaru na vifaa vingine.

Fungu la msaada wa kijeshi wa dola milioni 175 linajumuisha makombora ya kuongozwa kwa mifumo ya roketi za juu, au HIMARS, mifumo ya kuzuia silaha, na makombora ya kuzuia mionzi ya kasi, imesema na Pentagon na wizara ya mambo ya nje.

NANDY AKEMEA MAPEPO YA KUTAMANI KUWA YEYE KISA LULU DIVA KUTAKA KUMROGA… | BONGO 255

Leave A Reply