The House of Favourite Newspapers

Ratiba Ya Kombe la FA Hii Hapa, Simba vs Mwadui, Yanga na Prisons

0

 

 

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba itacheza Mwadui wakati Yanga ikitupwa kwa Tanzania Prisons katika raundi ya nne ya Kombe la FA itachezwa kati ya Januari 24-26, 2020, huku fainali yake ikipangwa kuchezwa Uwanja wa Mandela, Sumbawanga.

 

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano ya Kombe la FA mzunguko wa nne iliyopangwa leo Ijumaa inaonyesha mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam wenyewe watacheza Friends Rangers.

 

Vinara wa Ligi Kuu Simba watakuwa nyumbani kuivaa Mwadui ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu baada ya bao safi la Mathias Mdamu.

 

Yanga baada ya kuvunja rekodi ya Prisons ya kutokufungwa msimu huu katika ligi watakuwa nyumbani katika raundi hiyo kuwakaribisha maafande hao kwenye Uwanja wa Taifa.

 

Leave A Reply