Basila Aanika Vigezo Vipya Kushiriki Miss Tanzania – Video

Basila akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za Makampuni ya Global Group zilizopo, Sinza Mori jijini Dar. Kushoto ni Meneja wa Vipindi wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka. 

 

MWANDAAJI na msimamizi wa Shindano la Urembo nchini Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi ameanika vigezo vipya kwa washiriki wote wenye ndoto za kuwania shindano hilo kitaifa na hata kimataifa.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo akizungumza na Basila ofisini kwake.

 

Akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Mid Morning Fresh kinachoruka kupitia radio namba moja ya mtandaoni nchini Tanzania, +255 Global Radio, Basila amesema moja ya vigezo muhimu kwa sasa ni kila mshiriki kuwa na shughuli anayoifanya na kumuweka karibu na jamii inayomzunguka.

 

 

Basila akifanyiwa mahojiano ndani ya Studio za +255 Global Radio. 

Aidha, Basila kupitia Kampuni yake ya The Look amewataka washiriki wajitokeze kwa wingi na wasiogope kushiriki katika mashindano ya urembo ngazi ya taifa kwa kuhofia muonekano wao kwani vigezo ndivyo vitakavyoamua mshindi katika shindano hilo.

Mpigapicha wa Gazeti la Championi, Musa Mateja akimwonyesha gazeti hilo Basila.

Basila pia amezungumzia suala la zawadi kwa washindi walipita kuwa ni kutokana na kutokuwepo kwa wadhamini wa kutosha na kuomba wadhamini kujitokeza ili kuweza kutumia shindano hilo kama fursa ya kujitangaza.

 

Basila akifurahaia jambo katika picha ya pamoja na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ‘Jembe’ ofisini kwake.

 

Mwanukuzi ambaye pia ni mshindi wa mashindano hayo mwaka 1998 amesema licha ya changamoto zilizokuwepo malengo yake ni kuendelea kupeperusha bendera ya Miss Tanzania.

 

BASILA MWANUKUZI : NILINYIMWA PASSPORT YA KUSAFIRIA | MISS TANZANIA 1998


Loading...

Toa comment