The House of Favourite Newspapers

Ray J amjia juu Kanye West

0

Ray J amjia‘Ray J’

Los Angeles, Marekani

Mwanamuziki William Ray Norwood ‘Ray J’ hivi karibuni amemjia juu Kanye West baada ya kutoa video yake ya wimbo uitwao Famous akidai kuwa anaweza kumsababishia ndoa yake kutingishika.

Akizungumza na mtandao mmoja wa burudani, Ray J alisema kilichomkera kwenye video hiyo ni Kanye kumuweka karibu na mkewe Kim Kardashian huku akijua aliwahi kuwa na uhusiano naye, kitendo kinachoweza kumkera mpenzi wake wa sasa, Princess Love.

kanye-west-announces-swish-release-dateKanye West

“Kwa hili najaribu kuwa mpole kwelikweli,” Ray J aliuambia mtandao huo alipokuwa nyuma ya jukwaa kwenye tuzo za BET 2016 na kuongeza kwamba kwa sasa amechumbia hivyo anahofia ndoa yake isijekuingia ‘mdudu’.

Ray J na Princess Love walianzisha uhusiano uliodumu kwa muda wa miezi mitano mpaka sasa na Ray J na Kim Kardashian waliwahi kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi mwaka 2006 ambapo waliwahi kurekodi picha ya x pamoja.

Katika video hiyo, Kanye alitumia watu feki wanaofanana na mastaa ambapo aliwaweka katika ‘kapo’ wakiwa watupu huku Ray J akiwekwa na Kim Kardashian.

Leave A Reply