The House of Favourite Newspapers

Ray, JB kupima uzito kesho kabla ya kupasuana

Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Stephen ‘JB’

WAKALI  wa filamu nchini,  Vicent Kigosi ‘Ray’ na  Jacob  Stephen ‘JB’  wanatarajia kupima uzito kesho Jumamosi tayari kwa pambano lao la kukata na shoka linalotarajia kufanyika Aprili Mosi, mwaka huu (Sikukuu ya Pasaka) kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ray na JB watapanda ulingoni katika pambano hilo la raundi nane ambalo ni la  kumaliza ubishi kabla ya bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Hassan ‘Kiduku’ kupanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka Malawi, Chimwemwe Tchiota.

Akizungumza mtandao huu, Promota wa pambano hilo, Siraji Kaike alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo tayari yameshakamilika na kinachosubiriwa  kwa sasa  zoezi la kupima uzito litakalofanyika kesho Jumamosi kabla  ndonga zenyewe.

“Kila kitu kimeshakamilika kwa upande wa maandalizi, bondia kutoka  Malawi ameingia nchini  juzi Jumatano  tayari kwa pambano  ambalo linasubiriwa na wadau wengi kutokana na kuwepo mahasimu wa simba na Yanga ambao ni Ray na JB wakionyesha ubebe ndani ya ulingo.

“Hakuna asiyejua kama Ray ni shabiki wa Yanga na JB ni shabiki wa Simba hivyo mashabiki wa Simba na Yanvga watakuwa na kazi moja ya kuwasapoti watu katika pambano hilo kwa kujitokeza kwa wingi pale kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro,” alisema Kaike.

Nje ya mapambano hayo kutakuwa na  mapamabano ya utangulizi ambapo bondia Francis Miyeyusho Chichi Mawe atacheza Baina Mazora  , Charles Mashali akitarajia kuzichapa na Man  Chuga wakati Epson John ataonyesha umwamba na  Deo Njiku huku  Seba Temba akitatarajia kumalizana na Msafiri Msafiri.

Stori : Ibrahimu Mussa

 

Comments are closed.