The House of Favourite Newspapers

Rayuu Atoa Sababu Za Kutokufunga Mwezi Mtukufu

0
Msanii wa Bongo Muvi, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.

Stori: Mayasa Mariwata |Amani | Habari

MSANII kutoka Bongo Muvi, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo unaomsumbua umemfanya ashindwe kufunga kama alivyokuwa akifanya miaka ya nyuma.

Akizungumza na 3 Tamu, Rayuu amedai kuwa anaumia sana kutotimiza nguzo hiyo muhimu ya dini yake na anafanya kila awezalo kuhakikisha anautibu ugonjwa huo ili siku zijazo aweze kufunga.

“Nimekuwa nikijaribu kufunga lakini kabla siku haijaisha vizuri, vidonda vinatibuka hatari hivyo najikuta nikifungulia njiani, naumia sana kwa hali hii kwani napenda kufunga ila ndo hivyo sina jinsi,” alisema Rayuu.

 

Leave A Reply