The House of Favourite Newspapers

RC Amfanyia Kufuru Kiba

0

MAMBO mazuri! Mkuu wa Mkoa (RC) wa Iringa, Ali Hapi amemfanyia kufuru staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kwa kumpa kiwanja kwenye mkoa wake.

Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita baada ya mkuu huyo wa mkoa kwenda kwenye shoo aliyofanya Kiba kwenye ardhi ya mkoa huo aliozaliwa.

 

RC Hapi alimzawadia Kiba kiwanja hicho kwa sababu alifurahi kumuona amerudi nyumbani na Wana-Iringa walimpokea kwa mikono miwili.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, mmoja wa mameneja wa Kiba, Esi Mgimba alikiri Mkuu wa Mkoa wa Iringa kumpa kiwanja mwanamuziki wake na ataitolea ufafanuzi hivi karibuni.

 

“Ni kweli, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amempa Kiba kiwanja, lakini kwa sasa sitaweza kusema kina ukubwa gani na nitakitolea ufafanuzi siku za hivi karibuni.

“Kuhusu kabila, Kiba wengi wanajua kuwa ni mtu wa Kigoma, lakini siyo kweli, ni mtu wa Iringa kwa upande wa baba na kwa upande wa mama ndiyo ametokea Kigoma,” alisema meneja huyo.

 

Katika shoo hiyo, Kiba alikuwa na wanamuziki wenzake, Tunda Man, Tommy Flavour, Cheed, Christian Bella, Killy, Abdul Kiba, Ki2ga na DJ Feruu ambapo waliupamba vilivyo Uwanja wa Samora mkoani Morogoro kwa burudani ya kihistoria.

Shoo hiyo aliyoipa jina la Alikiba Unforgettable Tour, ataifanya kwenye mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro na kwingineko na atakuwa akipafomu akiwa na wasanii wengine kibao.

Leave A Reply