The House of Favourite Newspapers

RC Chalamila Akamata shehena ya bidhaa za magendo, madumu ya mafuta ya kupikia

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila Februari 21, 2024 ameueleza umma kupitia vyombo vya habari kukamatwa kwa shehena ya bidhaa za magendo, madumu ya mafuta ya kupikia zaidi ya elfu 11 Mbweni

RC Chalamila amesema Kushamiri kwa magendo ni kiashiria tosha kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma wanaohusika hivyo ameagiza Jeshi la polisi na TAKUKURU bila kupepesa macho kuwakamata mara moja watumishi wote wa bandari ndogo ya Mbweni wahojiwe kwa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe.

Aidha RC Chalamila amepongeza kazi nzuri inayofanywa na kikosi kazi katika ukanda mzima wa fukwe ya bahari ya hindi ambapo amesema kikosi kazi hicho kimejipanga vizuri kudhibiti biashara hizo za magendo ambazo zinatoka Zanzibar kuja Tanzania bara .


“ Hatuwezi kuruhusu bidhaa za magendo kupenya katika Mkoa huu kwa kuwa ni hatari kwa usalama wa watu na Taifa kwa Ujumla” amesistiza Chalamila

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema kati ya shehena za madumu ya mafuta zaidi ya elfu 11 madumu elfu 3 tu yalikuwa yamelipiwa mengine yote vibali vyake havikuonekana ndio maana yameshikiliwa na kuhifadhiwa katika Bandari kavu ya Ubungo.

Leave A Reply