The House of Favourite Newspapers

RC Homera: Wazee Jiepusheni na Vibinti

0

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera jana Oktoba 1, 2021 akiwa katika Kijiji cha Ihahi Mbarali amewatahadharisha wazee kujiepusha na mabinti wanaowanyemelea pindi wakipata tu kiinua mgongo chao baada ya kustaafu. Homera ameyasema hayo akizungumza na wazee kwenye Siku ya Wazee duniani.

 

“Mzee unamuacha Bibi pekee yake unakwenda kuchukua Binti mdogo. Wewe Babu ni Mzee lakini Binti anakuita Bebi! Bebi!, ujue hapo anataka hela yako. Anakuita ‘bebi’ si kwa sababu ya mvi ulizonazo bali anataka pesa ulizopata baada ya kustaafu ualimu.

 

“Kwa pesa za kustaafu, unamuacha Mzee mwenzako ambaye mmeishi toka miaka ya 40 pamoja na kwenda kuchukua Binti mdogo. Matokeo yake unatengeza mazingira magumu kwa Bibi mwenzako na mwisho badala ya kuishi vizuri na yule Binti unaharibikiwa na kupoteza maisha.

 

“Vijana (Mabinti) kwa sasa ni watukutu sana maana wakimng’ang’ania Mzee, atashughulishwa mpaka anapoteza maisha. Wazee jiepusheni sana na Mabinti wadogo wanaowanyemelea baada ya kupata pesa za kustaafu,” amesema Juma Homera, RC Mbeya.

Leave A Reply