The House of Favourite Newspapers

RC Kafulila Atoa siku 7 Mkataba na Mkandarasi Didia Co. Ltd Uvunjwe

0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ametoa siku 7 kwa mkataba kuvunjwa

MKUU wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ametoa muda wa siku saba kwa wakala wa Barabara mjini na vijijini (Tarula) Wilaya ya Meatu mkoani humo kuvunja mkataba na Mkandarasi Didia Co.ltd kutoka mkoani Shinyanga ambaye alikuwa anajenga barabara ya Mbaragane – Sulu.

 

Kafulila amefikia hatua hiyo leo baada ya kufanya ziara wilayani humo na kukagua ujenzi wa Barabara hiyo, na kubaini Mkandarasi huyo ameshindwa kutekeleza makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila

Katika mkataba huo, Mkandarasi huyo alitakiwa kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo kwa kipindi cha miezi sita, kutoka Novemba 2021 hadi Aprili 2022, ambapo mpaka sasa ameshindwa kukamilisha mradi huo.

Leave A Reply