RC KILIMANJARO APOKEA MSAADA WA MBOLEA TOKA GSM

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Onesmo Buswelu(kushoto)ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, akipokea msaada wa mifuko 70 ya Mbolea aina ya Urea kwa ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo,Msaada huo umetolewa na GSM Tanzania na kukabidhiwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa GSM Group,Matina Nkurlu(kulia)anaeshuhudia katikati ni Afisa mauzo wa kampuni hiyo kanda ya kaskazini Nurdin Mangenya.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Onesmo Buswelu (kulia) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, akihesabu mifuko  70 ya Mbolea aina ya Urea mara baada ya kukabidhiwa kama msaada kwa ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo.

 

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, amepokea msaada wa mifuko 70 ya Mbolea aina ya Urea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambapo mbolea hiyo ni kwa  ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani Kilimanjaro, Msaada huo umetolewa na GSM Tanzania na kukabidhiwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa GSM Group, Matina Nkurlu.

 

Toa comment