JIJI LA DAR LAPATA MANAIBU MEYA WAWILI, UKAWA WAUNGANA NA CCM

Hatimaye Jiji la Dar es Salaam limepata Manaibu Meya wawili baada ya wagombea wawili wa nafasi hiyo kulingana kura wakati wa uchaguzi uliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

 

Wagombea hao ambao ni Mariam Lulida (CCM) na Ally Haroub (CUF), kila mmoja amepata kura 12, ambapo sasa wataongoza kwa kupokezana kila baada ya miezi mitatu kuanzia Desemba 30, 2018.

 

Kabla ya uchaguzi huo, Mvutano mkali uliibuka katika ambapo wajumbe walipinga mkutano kutawaliwa na idadi kubwa ya askari tofauti na wajumbe wenye haki ya kupiga kura.

 

Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa baraza la madiwani juu ya uchaguzi wa naibu meya ambao akidi ya wajumbe imefanana 13 kwa 13 umegubikwa na mvutano baada ya pande zote mbili kutaka uchaguzi huo uaarishwe kwa madai ya kuhofia haki kutotendeka lakini baadaye ulifanyika na matokeo yakatangazwa.

 

Akizungumza wakati wakutangaza uamuzi huo ulioafikiwa na wajumbe wa baraza hilo, Mstahiki Meya  Isaya Mwita amesema kuwa kutokana na hali hiyo kila mmoja ataongoza kwa kipindi cha miezi mitatu hadi Juni 30 mwaka 2019.

Tumefikia uamuzi huo kwani viongozi wamechaguliwa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya waanchi bila kujali vyama vyao, kuwepo kwa viongozi wa vyama viwili tofauti haitawakosesha wananchi maendeleo kwakuwa wote wamechaguliwa kwa lengo la kuwatumikia wakazi wa jijini hapa“, amesema Meya Mwita.

 

Kabla ya kufanyika kwa maamuzi hayo, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sita alitoa hoja baada ya kuwepo kwa mvutano mkali kuwa baraza lijigeuze kamati ili kufanya maamuzi ambayo yatakuwa na maslahi kwa wananchi kuliko kuendelea na mabishano.

 

“ Ndugu mwenyekiti hakuna haja ya kuendelea kubishana, wote hapa tunafanya kazi kwa ajili ya wanachi wa jijini hapa, ningeshauri tujigeuze kamati ili kufikia muafaka wa jambo hili”.

 

Baada ya hoja hiyo kutolewa, wajumbe wa baraza hilo walikubaliana kama kamati, ambapo baada ya nusu saa walirudi kuwa baraza na hivyo Meya Mwita kutoa maamuzi ya uchaguzi huo. Uchaguzi huo umefanyika leo ikiwa ni baada ya aliyekuwa Naibu Meya Mussa Kafana kujiuzulu nafasi yake na kujiunga na CCM Septemba mwaka huu.

BREAKING: RAIS MAGUFULI Atoa Msamaha Kwa Wafungwa 4477

Toa comment