The House of Favourite Newspapers

Kunenge Awapongeza Wauguzi Dar

0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Aboubakar Kunenge, amewapongeza wauguzi wa mkoa huo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kuokoa maisha ya wananchi, jambo linalosaidia kupunguza vifo.

 

Amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amewahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa uwezo wao wote na kuwaahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega.

Aidha amesema serikali ya Rais John Magufuli imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuboresha huduma za afya kupitia ujenzi wa hospital, zahanati, vituo vya afya na kununua vifaa tiba ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.

 

Pia amesema anafurahi kuona hata zile kelele za wananchi kuhusu lugha chafu kwa wafanyakazi mahospitalini zimepungua na badala yake wauguzi wamekuwa na lugha za upendo kwa wagonjwa, jambo linalotia faraja.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dr. Rashid Mfaume, amewaalika wananchi kujitokeza kwenye Viwanja vya Karimjee kujionea kazi zinazofanywa na wauguzi wa mkoa huo.

 

Amewaahidi wananchi kutegemea mabadiliko makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa serikali ya mkoa imejizatiti kutoa huduma Bbra na zenye tija.

 

Leave A Reply