MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema atampa pesa kiasi cha Tsh milioni tano, mama mzazi wa aliyekuwa Rapa wa Bongo, marehemu Golden Jacob Mbunda ‘Godzilla’ ili zimsaidie katika kuwatunza watoto wa marehemu.
Makonda amesema hayo leo Jumamosi, Februari 16, 2019 katika Uwanja wa Salasala wakati akitoa salam za pole kwa familia, ndugu na wasanii kwa kuondokea na msanii huyo aliyeaga dunia usiku wa kuamkia Februari 13, mwaka huu.
Mwili wa Zilla utazikwa leo katika Makaburi ya Kinondi jijini Dar es Salaam.
Comments are closed.