RC Makonda: “Fungueni Hoteli, Mliokimbia Dar Rudini Tupige Kazi” -Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda leo Machi 19, 2020 amewasihi Wafanyabiashara na wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaanza kufungua biashara zao na kuchapa kazi ili kujenga uchumi wa nchi.

 

Akizungumza leo alipofanya ziara sehemu linapojengwa daraja la Selander amesema “ Rais Magufuli ametupa siku 3 za shukrani tumshukuru Mungu wetu, yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, kupitia hizo kila mmoja atafanya ibada yake ya kumshukuru Mungu”.

 

Aidha, ameongeza “Nimeomba inapofika Jumapili kila mmoja apige shangwe na vigelegele na kila aina ya fujo anayoijua, ikiwa ni ishara ya kwamba Mungu wetu ametushindia. Kwa hiyo kama una disko lako nyumbani washa, nimekupa uhuru, kama unaweza kwenda sehemu ya bahari kuogelea fanya”

Toa comment