RC Makonda: Wabunge Dar Wahesabu Maumivu 2020 – Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam wasiofanya ziara na kutatua kero za wananchi mwaka 2020 wahesabu maumivu.

“Mimi kama nimejenga majengo basi na wao wahangaike kuleta madawati lakini wakisubiri uchaguzi (wa 2020) mimi nikiwepo wahesabu maumivu,” amesema Makonda.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 8, 2019 katika uzinduzi wa ofisi za walimu Shule ya Msingi Vijibweni Wilaya ya Kigamboni zilizojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya CRJE (East Africa) Limited ya China.


“Wako wabunge wanaojiona wa kimataifa hawahangaiki na kero za wananchi wala hawataki kufanya ziara wanasubiri wakapige kelele bungeni na kujirekodi,” amesema Makonda.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema wabunge hao wamezoea ukibaki mwaka mmoja kuelekea uchaguzi mkuu ndio huanza kujipitisha na kusikiliza kero za wananchi, akibainisha kuwa safari hii wahesabu maumivu.

Meneja ujenzi tawi kampuni hiyo, Bai Hao Chein amesema wameamua kujenga ofisi hiyo ili kupanua kiwango cha elimu.

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

Loading...

Toa comment