The House of Favourite Newspapers

RC, SINGIDA AWATAKA WAKULIMA, WAFANYABIASHARA KUWEKA FEDHA BENKI

Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi.
Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akionyesha risiti za benki ya NMB.

 

WAKULIMA na wafanyabiashara wametakiwa kutumia taasisi za kifedha hasa mabenki kutunza fedha ili kuepuka matumizi yasiyo ya lazima, badala ya kuweka katika vibubu ndani ya nyumba, jambo ambalo ni hatari.

 

Akizungumza katika uzinduzi wa wakala wa benki ya NMB, Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alisema kuwa wakulima hasa vijana hujipatia fedha nyingi kutokana na mauzo ya vitunguu na alizeti wakati wa mavuno, hivyo ni vyema wakaweka fedha zao benki kwa ajili ya usalama na maendeleo yao ya baadaye.

 

“Ufunguzi wa wakala huu nasema Singida ni njema tena njema sana, Singida siyo ile ya miaka iliyopita, hivi sasa imebadilika hivyo vijana lazima wabadilike kwa sababu wapo jirani na makao makuu ya nchi, yaliyopo jijini Dodoma,” alisema Dk. Nchimbi.

 

Awali katika uzinduzi huo, Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi alisema wakala huyo kutoka kampuni ya GMM Group anakuwa wakala wa 6,001, lengo likiwa ni kufikisha mawakala 10,000 mwaka huu nchi nzima ili kuhakikisha jamii yote hadi vijijini inafikiwa na huduma za kifedha.

 

Comments are closed.