The House of Favourite Newspapers

Real Madrid Yatinga Robo Fainali Baada ya Miaka 3

0

MABINGWA wa kihistoria wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, Klabu ya Real Madrid imetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada usiku wa kuamkia leo kuitoa klabu ya Atalanta ya Italia kwa kuifunga mabao 3-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1 kwenye michezo miwili ya mtoano.

 

 

Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Karim Benzema aliyefunga dakika ya 34, Sergio Ramos aliyefunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 60 kabla ya Marco Asensio kufunga bao la tatu dakika ya 84 ikiwa ni dakika moja kupita Luis Muriel kuwafungia Atalanta bao la kufutia machozi.

 

 

Bao alilofunga mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema limemfanya afikishe mabao 21 msimu huu kwenye michuano yote huku akifunga mabao 6 mfululizo katika michezo mitano ya mwisho aliyocheza baada ya kupona majeraha yake na kurejea kikosini.

 

 

Real Mardi imefuzu hatua hiyo kwa mara ya kwanza baada ya misimu mitatu kupita jambo ambalo limemfanya kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane kuwapongeza wachezaji wake kwa kufanya kazi nzuri.

 

 

Zidane amesema “Nimewapongeza wachezaji kwasababu walikuwa na mchezo mzuri mwanzo hadi mwisho tena dhidi ya upande ambao ulikuwa unamatumizi makubwa ya nguvu. Tulihitaji kujilinda vizuri na tuliweza kucheza mchezo wetu tulivyokuwa na umiliki wa mpira”.

 

 

“Kikawaida wanatengenezaga nafasi nyingi sana, lakini leo hawakuweza. Tulicheza vizuri na tulionekana wazuri hasa kwenda mbele kushambulia”.

 

 

Kwa upande wa kocha wa Atalanta, Gian Piere Gasperini amesema “Hatuwezi kukubali kufanya makosa na kuwazadia mabao wapinzani wetu, tulitaka tufanye vizuri zaidi. Ni huzuni. Lakini siku zote ni fursa nzuri kwa kila mtu kupata uzoefu”.

 

 

“Tumepata nafasi ya kucheza na miongoni mwa timu bora barani Ulaya, tumefanya vizuri msimu huu na tumehuzunika hususani kwa michezo hii miwili ya mwisho”.

 

 

Huu ulikuwa ni msimu wa pili kwa Atalanta kushiriki michuano hiyo mikubwa Duniani na kufanikiwa kuandika historia ya kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo lakini kushindwa kusonga mbele na kutinga hatua ya nusu fainali.

 

 

Madrid imeungana na Borussia Dortmund ya Ujerumani, FC Porto ya Ureno, PSG ya Ufaransa, Manchester City na Liverpool zote za England kutinga hatua ya robo fainali.

 

 

Droo ya nani kucheza na nani kwenye hatua ya robo fainali pamoja na ile ya nusu fainali inatazamiwa kupangwa siku ya Ijumaa ya tarehe 19 Machi 2021 nchni Uswizi.

Leave A Reply