The House of Favourite Newspapers

Wanamgambo ‘Wawakata Vichwa Watoto’

0


KWA mujibu wa Shirika la Kimataifa la Save the Children linasema watoto wadogo wa hadi miaka 11 wanauawa kwa kuchinjwa na wanamgambo wa Kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji.

 

 

Mwanamke mmoja ameliambia Save the Children kwamba alishuhudia mtoto wake aliyekua na umri wa miaka 12 akiuawa karibu na mahali alipokuwa amejificha na watoto wake wengine.

 

 

“Baada ya mwanangu kuuawa, tulibaini ni hatari kuendelea kuishi katika kijiji chetu. Tulikimbili anyumbani kwa baba yangu katika kijiji kingine, lakini baada ya siku chache mashambulio yakaanza tena huko pia,” alisema.

 

 

Zaidi ya watu 2,500 wameuawa na wengine 700,000 wametoroka makwao katika mkoa wa Cabo Delgado ulio na utajiri mkubwa wa gesi na mafuta tangu mashambulio ya wanamgambo yalipoanza mwaka 2017.

Leave A Reply