The House of Favourite Newspapers

Kiungo Anusurika Panga Simba

0

MUDA na wakati wowote Simba itamuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wake mshambuliaji Miraji Athumani ‘Sheva’ wa kuendelea kukipiga Msimbazi.

 

Awali kiungo huyo alikuwa kwenye orodha ya wachezaji watakaochwa katika kuelekea usajili wa msimu ujao ambao wanajiandaa na michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara.

 

Simba inadaiwa kuachana na wachezaji wake watatu ambao kiungo Mkenya Francis Kahata ambaye mkataba wake umeisha na tayari asharudi kwao Kenya wengine ni Ibrahim Ajibu na Gadiel Michael.

 

Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba, kimeliambia Championi Jumatano kuwa, Sheva amebakishwa kuendelea kukipiga katika timu hiyo baada ya kocha Mfaransa Didier Gomes kupendekeza abaki.

 

Kilisema kuwa kiungo huyo amebakishwa baada ya kocha kushawishika na kiwango chake akiamini kitaongezeka hapo baadaye baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha aliyoyapata.

 

Chanzo hicho kiliongeza kuwa kikubwa kocha hataki kuwaacha rundo la wachezaji wengi, hivyo atawabakisha wale ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri.

 

“Sheva ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji ambao kocha atawaacha katika usajili wa msimu ujao, ni baada ya benchi la ufundi kupendekeza kumbakisha Simba.

 

Na anaachwa baada ya tathimini kubwa iliyofanywa na benchi la ufundi wakiamini bado Sheva yupo vizuri, lakini kiwango kilishuka hapa katikati baada ya kupata majeraha ambayo hivi sasa amepona.

 

“Sheva ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu pamoja na akina Ajibu na Gadiel ambao hao tayari wameachwa,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Simba kwa kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ hivi karibuni alifanya mazungumzo na gazeti akizungumzia usajili alisema kuwa: “Masuala yote yanayohusu usajili wamewaachia benchi la ufundi.“Na ripoti ya usajili bado haijakabidhiwa kwa uongozi mara baada ya kuipata tutaanza uifanyia kazi sehemu ya utawala.”

Stori na Wilbert Molandi, Dar es Salaam

 

Leave A Reply