The House of Favourite Newspapers

Rihanna akasirika kufananishwa na Karrueche

0

best-beauty-rihannaMwanamuziki Rihanna.

NEW YORK, Marekani
MWANAMUZIKI Rihanna, amekasirishwa na kitendo cha ‘ex’ wake, Chris Brown kumfananisha na wanawake wengine aliowahi kutoka nao kimapenzi.

Hivi karibuni Chris alipost kwenye Instagram picha aliyoiunganisha ikimuonyesha akiwa na wanawake wanne tofautitofauti akifurahi nao sehemu mbalimbali, mmojawao akiwa ni Rihanna, wengine walikuwa Karrueche Tran, Draya Michele na Jasmine Sanders.

Karrueche-TranMwanamitindo  Karrueche Tran.

Rihanna amesema kitendo hicho ni kama Chris amemvunjia heshima kwa kuwa yeye ni mwanamke aliye juu zaidi kati ya wote waliowahi kutoka na Chris, hivyo hastahili kufananishwa na mwanamke yeyote kati ya hao.

“Hajapendezewa na kitendo cha kulinganishwa na wanawake wengine wa Chris, hasa huyu Karrueche,” alisema rafiki wa karibu wa Rihanna na kuendelea: “Hataki kumvunjia heshima mtu yeyote, lakini Riri ni zaidi ya wote hao. Kila sehemu yeye ataendelea kung’ara kama almasi na haitabadilika kuwa ni zaidi ya wanawake wote aliowahi kuwa nao Chris.”

Leave A Reply