Shein atangazwa mshindi wa urais Zanzibar
Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohammed Shein.
Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.Dkt Ali Mohammed Shein atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar akiwa na kura 299,982.
Mgombea wa CCM, Dkt Ali Mohammed Shein akikabidhiwa cheti cha ushindi wa urais.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha akiongea jambo wakati akitangaza matokeo.
Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua rais. Majina yao ndiyo haya:
1 | Khamis Iddi Lila | ACT-W |
2 | Juma Ali Khatib | ADA-TADEA |
3 | Hamad Rashid Mohamed | ADC |
4 | Said Soud Said | AFP |
5 | Ali Khatib Ali | CCK |
6 | Ali Mohamed Shein | CCM |
7 | Mohammed Massoud Rashid | CHAUMMA |
8 | Seif Sharif Hamad | CUF |
9 | Taibu Mussa Juma | DM |
10 | Abdalla Kombo Khamis | DP |
11 | Kassim Bakar Aly | JAHAZI |
12 | Seif Ali Iddi | NRA |
13 | Issa Mohammed Zonga | SAU |
14 | Hafidh Hassan Suleiman | TLP |