The House of Favourite Newspapers

Roboti Inayoweza Kushiriki Ngono Kutengezwa

roboti-inayoweza-kushiriki-ngono-kutengezwa-1 HII teknolojia sasa imekuwa too much! Kila kukicha wenzetu wazungu wamekuwa wakibuni vitu vipya tofauti kabisa na fikira za kawaida za kibinadamu na kuendelea kuushangaza ulimwengu na viumbe vyake, hatujui tunaelekea wapi na hizi teknolojia zinazobuniwa na wenzetu kila siku.

Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? Ungefunga ndoa na roboti? Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo?

Haya ni baadhi ya maswali machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika Chuo Kikuu cha Goldsmith mjini London nchini Uingereza baada ya Serikali ya Malaysia ambayo ndio iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku.

Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina na hapakuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.

roboti-inayoweza-kushiriki-ngono-kutengezwa-2

Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono (roboti) ilidai kwamba itatengeza roboti wanaoweza kushiriki ngono na mwenye akili bandia kama za binadamu mwaka ujao. Uzinduzi huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.

Alitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono. ”Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya”. Alisema.

roboti-inayoweza-kushiriki-ngono-kutengezwa-3Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima na hailalamiki alisema.

Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga nao ndoa. Wanaharakati wa masuala ya ndoa nchini humo wameeleza kuwa, mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususana wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binaadamu.

Lady Jaydee Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya , Agoma Kumsaidia Ray C

Comments are closed.