The House of Favourite Newspapers

Roma: ‘BASATA Mtaniua Njaa Jamani’, Mwanae Akosa Ada Ya Shule

Staa namba moja katika Hip Hop kwa sasa nchini, Roma Mkatoliki.

STAA namba moja katika Hip Hop kwa sasa nchini, Roma Mkatoliki amefunguka kwa mara ya kwanza ikiwa ni mwezi mmoja toka afungiwe na Baraza la Sanaa la Taifa kujihusisha na shughuli za sanaa kutokana na kudaiwa kutoa wimbo ‘Kibamia’ ambao hauna maadili.

 

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatato hii, Roma akiwa na mwanae, Ivan amesema anawaomba BASATA kumpungia adhabu kwani hali yake ya kiuchumi siyo nzuri.

 

“Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee,” alisema Roma.

 

Aliongeza,”Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja,

 

Akiwa katika mahojiano hayo na mtoto wake, Ivan aliulizwa na matangazaji wakipindi hicho kwanini hakwenda shule, na mtoto alisema hajaenda shule kutokana na tatizo la ada.

 

 

Serikali Yamfungia Roma Kisa ‘KIBAMIA’

 

Comments are closed.