The House of Favourite Newspapers

Rooney Akatwa Mshahara wa Wiki Mbili

0
Wayne Rooney.

KLABU ya Everton iliyo katika ligi kuu ya Uingereza (EPL), imempiga faini mchezaji wake, Wayne Rooney, kwa kumkata mshahara wa wiki mbili kutokana na kutiwa hatiani na mahakama kwa kuendesha gari akiwa amelewa.

Everton ina nia ya kuipeleka fedha hiyo inayokadiriwa kuwa Paundi 300,000 (Sh. Milioni 900) kwenye miradi ya kijamii inayohitaji misaada. Rooney mwenyewe aliye na umri wa miaka 31, amekiri kosa hilo baada ya kuambiwa adhabu hiyo.
Mchezaji huyo alifikishwa mahakamani Jumatatu wiki hii baada ya kukamatwa Septemba 1 mwaka huu akiwa anaendesha gari kwa kasi iliyokuwa mara tatu zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya England alipigwa marufuku kuendesha gari kwa miaka miwili na alihukumiwa kufanya kazi za jamii bila malipo mara 100 katika kipindi cha miezi 12.
Isitoshe, mchezaji huyo aliamriwa kulipa Paundi 170 (Sh. 515,000) zikiwa gharama ya kuendesha kesi hiyo.

Simba Yafanya Mazoezi ya Mwisho Kabla ya Kuwavaa Mbao FC

Leave A Reply