The House of Favourite Newspapers

BAADA YA MTOTO WA MOBETO, MAPACHA WENGINE WAIBUKA KUTOKA BURUNDI!

0

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, wakati sakata la mwanamitindo, Hamisa Mobeto, kuzaa na mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, likiwa bado bichi kabisa na halijafutika akilini mwa watu, mwanamke mwingine kutoka Burundi ameibuka na kudai ana watoto mapacha wa mwanamuziki huyo.

Ishu hiyo imeanzia mitandaoni baada ya mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Jesca, kuposti picha ya Zari anayedai alikuwa shoga ake, na kumshushia kichambohevi’, huku akimtuhumu kuwa alimpora mwanamuziki huyo, kwani mara ya kwanza alikuwa ni wake na yeye alikuwa akimuita shemeji.

Baada ya kumchamba Zari, akaposti tena picha yake akiwa na watoto wake mapacha anaodai kuzaa na mzazi mwenziye Zari, akimuomba aje awachukue watoto wake.

Mpaka sasa bado mwanamuziki huyo ambaye ni baba watatu kwa sasa, hajathibitisha kuwa anamfahamu mwanamke huyo na hao watoto ni wa kwake kweli.

NA ISRI MOHAMED/GPL

KIMENUKA!! Kumbe Diamond Alizaa Mapacha na Shoga Ake Zari

Leave A Reply