The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree Alamba Dili Kama la Rick Ross, DJ Khaled

0

NA ANDREW CARLOS | IJUMAA WIKIENDA | Over Ze Weekend

MKALI wa Ngoma ya Up In The Air, anayefahamika zaidi kwa jina la Rosa Ree amefunguka kuwa shavu la ubalozi wa kinywaji cha Belaire alilopata pamoja na wanamuziki kutoka Marekani, Rick Ross na DJ Khaled limemuongezea ujasiri na kuamini kila kitu kinawezekana.

Akichonga na Over Ze Weekend, Rosa Ree ambaye yupo chini ya Lebo ya The Industry alisema kuwa, kwake hiyo ni hatua kubwa na jambo la kumtia moyo kwamba anaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya hilo ikiwa tu ataendelea kukomaa zaidi.

“Unajua si kitu kidogo kuwa balozi na kina Rick Ross, hapa inamaanisha mimi pia ninamega kwenye sahani wanapokula wao, kwangu hili ni jambo kubwa sana,” alisema Rosa Ree.

Leave A Reply