The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree na Changamoto ya Kuombwa Penzi

0

NA ALLY KATALAMBULA | UWAZISHOWBIZ

ROSA Ree, ni moja ya majina ya marapa wa kike ambao kwa sasa wameliteka gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo.

Anavyorap unaweza kusema yupo Bongo bahati mbaya na alifaa kuwa mbele, hata hivyo ni mautundu tu maana mwanadada huyu ambaye jina lake la kuzaliwa ni Rosary Robert anaasili ya Kichaga na ni mzaliwa wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Tangu aanze kusikika kwenye media si zaidi ya miaka miwili, lakini amebahatika kusikika kwenye ngoma kadhaa kali na miongoni ni One Time, Up To The Air na One Time Remix aliyofanya na Kaligraph Jones kutoka Kenya.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Rosa Ree ambaye yupo chini ya Lebal ya The Industry inayomilikiwa na Kundi la Navy Kenzo, amefunguka kuwa matumaini mapya katika muziki wake alianza kuyapata baada ya kukutana na Aika na Nahreel mabosi wa lebal hiyo alipokwenda kufanya ngoma katika studio yao.

Lakini kabla anasema alikuwa ‘akihustle’ kwenye studio tofauti kutafuta nafasi ya kurekodi ama kusainiwa lebal bila mafanikio na wazazi wake wamekuwa wakimsapoti tangu walipogundua kuwa anakipaji hicho cha kurap mpaka sasa!

CHANGAMOTO ALIZOKUTANA NAZO

Rosa Ree ameiambia Uwazi Showbiz kuwa akiwa msanii chipukizi alikutana na changamoto nyingi, kama kukosa studio ya kurekodia kwa wakati muafaka, nyimbo zake kutosikika na kukosa usimamizi.

Hata hivyo, tofauti na marapa wengi wa kike, Rosa Ree amefunguka kuwa hajawahi kupambana na changamoto za maprodyuza wala wadau wa muziki kumtaka kimapenzi kwa ajili ya kumsaidia. Hata hivyo, kwake hiyo si changamoto ya kumzuia kusonga mbele.

SIKIA ANACHOJIVUNIA

Rosa Ree: Kiukweli najivunia sana kuwa na prodyuza bora Afrika Mashariki, Nahreel. Amenipa ‘confidence’ ya kufanya jambo lolote lile kwenye biti na hata usimamizi wake na Nahreel ni bora.

Uwazi Showbiz: Umewahi kufikiria ukitoka The Industry utapenda kufanya kazi na lebal gani nyingine?

Rosa Ree: Sijafikiria jambo kama hilo mpaka sasa. Ninachowaza ni kufanya kazi na The Industry tu!

Uwazi Showbiz: Kingine?

Rosa Ree: Kuwa na kipaji cha muziki. Ambapo ninauwezo wa kufikisha hisia zangu na za watu wengine kwenye jamii, pamoja na kuwaunganisha watu pamoja kupitia muziki.

HIKI HATAKISAHAU

Uwazi Showbiz: Mpaka sasa kuna jambo lolote kubwa ambalo umekutananalo ambalo huwezi kulisahau kwenye ‘hustle’ zako za muziki?

Rosa Ree: Mh! Kiukweli labda tulivyokamatwa na polisi wakati tunashuti video ya Wimbo wa Up To The Air. Kuna mambo yalitokea lokesheni tukakamatwa, lakini hiyo ilikuwa ni changamoto ambayo tuliivuka na kusonga mbele na mambo mengine yanaendelea kwa sasa.

NI BALOZI WA BELAIRE

Rosa Ree alizidi kufunguka pia kuwa yeye ni miongoni mwa mabalozi wa kinywaji kiitwacho Belaire akiwa pamoja na wasanii kutoka Marekani, Rick Ross na DJ Khareed.

Uwazi Showbiz: Una malengo gani kwenye muziki?

Rosa Ree: Kufika mbali zaidi ya hapa nilipo.

Uwazi Showbiz: Ukiachana na muziki upo ndani ya uhusiano wa kimapenzi?

Rosa Ree: Kuhusu mambo nje ya muziki sipo tayari kuyaweka wazi kwa sasa. Muda sahihi ukifika nitaweka wazi.

Uwazi Showbiz: Kama unalo la kumalizia hii ni nafasi kwako.

Rosa Ree: Nashukuru kwa media kunipa sapoti, wapenzi wa muziki na watu wote. Niambie tu sitawaangusha kikubwa wasichoke kunipa sapoti, kuhusu ujio mpya ni sapraizi, watu wawe tu mkao wa kula.

=======================

Harmonize Ataja Sababu za Kutoendana na Wolper, Azungumzia Umaarufu wa Harmorapa

Leave A Reply