The House of Favourite Newspapers

ROSTAM: TUNAKESHA TUKIFUNGA JUMLA JUMLA

WAKALI wawili wasioshikika kwenye Muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki pamoja na Stamina wanaounda Kundi la Rostam wamesema kuwa, kuelekea mkesha wa Mwaka Mpya watahakikisha wanafanya shoo bab’kubwa inayotambulika kama Tunafunga Jumla Jumla, Desemba 31, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Amani, Roma alisema, kila mwaka huwa habahatishi katika kufanya shoo za kufunga mwaka.

 

“Kama mtakumbuka katika mkesha wa Mwaka Mpya ile mwaka jana niliingia na ‘crane’ ambayo ilinibeba juu na kunishusha ndani ya Dar Live katika shoo ya Nishushe Dar Live. Sasa basi mwaka huu nitakuwa na kichaa wangu Stamina tutakavyoshuka njoo ujionee mwenyewe usije kusimuliwa,” alisema Roma.

 

Naye Stamina alisema, Dar Live mara yake ya mwisho kupiga shoo ilikuwa siku hiyohiyo na aliingia akiwa ndani ya Bajaj jukwaani hivyo mashabiki wategemee kitu cha tofauti mwaka huu.

 

“Sina maneno mengi, maneno siku zote huwa jukwaani, usikose mtu wangu!” Alisema Stamina kwa kifupi.

Comments are closed.