The House of Favourite Newspapers

Rosti la Tambi na Kuku wa Kukaanga!

LEO kwenye mapishi tutaona jinsi ya kupika tambi aina ya super get ambazo ni tamu na ni nzuri kula kama mlo wa mchana au usiku ingawa wapo wanaokula kama kitafunwa.

MAHITAJI:

-Nyanya

-Kitunguu maji

-Kitunguu swaumu

-Tambi

-Mafuta ya kupikia

Jinsi ya kupika

Andaa nyanya zako na kitunguu swaumu kama kawaida, anza kwa kubandika mafuta kwanza kwenye  kikaango kisha weka kitunguu kikaange

kwenye mafuta kiasi kisha weka kitunguu swaumu na nyanya, unga ukimaliza weka mchuzi kiasi kisha weka tambi ambazo umeshazichemsha kidogo kwenye maji na kuzichuja.

Ukishaweka koroga vizuri ili zishikane na nyanya zako ulizoandaa.

Baada ya hapo epua zitakuwa tayari kwa kuliwa, unachotakiwa ni kukaanga sasa kitoweo cha kuku, kisha weka mezani kwa ajili ya kula sasa.

Na Hamida Hassan. 

Comments are closed.