The House of Favourite Newspapers

Rotimi Atamfikisha V-Money….

0

Ni takriban miezi miwili tangu mwanadada kutoka Bongo Flevani, Vanessa Hau Mdee ‘Vee Money’ alipoanza kushika vyombo vya habari akiripotiwa kuwa kwenye penzi matata na staa wa Marekani, mwenye asili ya nchini Nigeria, Olurotimi Akinosho maarufu kama Rotimi.

 

Rotimi ni bonge moja la staa wa tamthiliya, sinema, muziki na mitindo wa nchini Marekani.

Huyu jamaa mpya wa Vee ameshaonekana kwenye sinema kubwa kama Divergent ambayo iliachiwa mwaka 2014 akiwa na mastaa wengine kibao wa mamtoni.

Pia ameuza sura sana kwenye tamthiliya kubwa kama Boss na Power ambayo yupo na mkongwe wa Hip Hop wa Marekani, Curtis Jackson III ‘50 Cent’.

 

KIMAFANIKIO

Kwa mafanikio aliyonayo Rotimi kwenye sekta ya sanaa, yanatosha kabisa kwa Vee kutimiza ndoto zake za kimuziki. Vee amepata mtu ambaye anaweza kukutana na wasanii wakubwa duniani na hata mameneja wakubwa, jambo ambalo linaweza kumpeleka mbali mno yeye na Bongo Fleva kwa ujumla kama mastaa wa muziki huu watamtumia Vee kupata koneksheni.

 

Vee atakapokutana na hao mastaa wakubwa kwa mgongo wa Rotimi, pasi na shaka, watamuelewa na hata kukubali kufanya naye kazi kwani mbali na kumuona ni ‘mtu’ wa staa mwenzao ambaye wanamfahamu kwa ukaribu zaidi, pia kipaji cha Vee ni kikubwa.

 

KUTEMBELEA STUDIO KUBWA

Katika kuanza kuonesha mwanga, hivi karibuni, Rotimi alikuwa ndani ya studio zinazotajwa kuwa kubwa duniani kwa sasa za Tyler Perry Studios zilizopo Atlanta- Georgia nchini Marekani. Ndani ya studio hizo, Rotimi hakwenda mwenyewe, aliambatana na Vee, jambo ambalo ni zuri zaidi kwa soko la muziki wa Vee na Bongo Fleva kwani ndani ya studio hizo anaweza kukutana na watayarishaji au wachawi wakubwa wa muziki na filamu na wakafanya naye kazi. Najua Vee anaweza vyote; kuimba kwa maana ya muziki na kuigiza.

 

KUFANYA KAZI NA KAMPUNI KUBWA

Ni juzikati tu ambapo Vee aliachia bonge moja la ngoma ambalo ni remix ya ngoma yake ya Never Ever.

Ngoma hiyo, Vee aliifanya zamani kwa Prodyuza Nahreel, ilifanya poa sana kwa kipindi hicho.

Ngoma hiyo ameirudia tofauti mno huku akiwashirikisha wasanii maarufu duniani kama Frederic Gassita wa nchini Gabon na The London Symphony Orchestra wa Uingereza ambao ni washindi wa Tuzo za Grammy kwa miaka isiyopungua nane kila zifanyikapo.

 

Kitendo cha kufanya ngoma hiyo na wakali hao, ni miongoni mwa fursa alizozipata kupitia Rotimi na anafurahia kuendelea kufanya kazi na watu hao kwani anapata nafasi ya kutambulika zaidi kimataifa na kuzidi kuwashawishi hata wanaotaka kufanya naye kazi.

Kwenye intavyuu mbalimbali, Vee amesikika akimsifia Rotimi akimtaja kuwa ndiye mwanaume ambaye atamfikisha mbali mno kiasi cha kumuita mume wake hata kabla ya ndoa. Siyo jambo la kawaida kwa staa kuz-ama kwenye mapenzi kiasi hicho.

 

Vee anafurahia maisha wanay-oishi, wanao-nekana wenye furaha kwani kila wanapo-onekana kwenye mita-ndao ya kijamii, wao ni vicheko tu huku wakiwa kwenye pati kubwa-kubwa na mastaa wa nchini Marekani. Maisha yanataka nini tena?

Jambo hili si tu kwamba linampa furaha Vee, lakini linatafsiriwa kama kufunguka kwa milango ya baraka.

 

VYOMBO VYA HABARI MAREKANI

Vee kwa sasa ameanza kushika vichwa vya habari za burudani nchini Marekani kutokana na penzi lake hilo kuonekana limepamba moto kiasi cha kutawala mitandao ya kijamii kwa kasi dunia nzima.

Leave A Reply