Rubani Azirai Akiendesha Ndege, Mwanafuzi Aokoa Jahazi

RUBANI mwanafunzi nchini Australia ameitua ndege salama baada mwalimu wake kuzirai akiwa angani. Max Sylvester, mkazi wa magharibi mwa Australia aliwasiliana kwa dharura na waelekezaji wa ndege saa moja baada ya mwalimu wake kuzirai wakiwa angani juzi Jumamosi iliyopita Agosti 31.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, wahudumu hao walimsaidia mwanafunzi huyo kuitua ndege salama katika Uwanja wa Ndege wa Perth ambapo alisifiwa kwa kuchukua hatua ya haraka na kuwa mtulivu wakati wa tukio hilo.
Katika mawasiliano yaliyorekodiwa na baadaye kuwekwa wazi hadharani, Slivester alielezea ilivyokuwa hali ya mwalimu wake kabla ya kuchukua jukumu la kuindesha ndege hiyo.
“Kwanza aliniegemea katika bega langu, nilijaribu kumwamsha lakini hakushtuka,” mwanafunzi huyo aliwaambia mafundi wa mitambo.
Alipoulizwa kama anajua jinsi ya kuendesha ndege aina ya Cessna, mwanafunzi huyo alijibu:  “Hili ni somo langu la kwanza.”
Baada ya kupaa juu ya Uwanja wa Ndege wa Perth kwa karibu saa moja akifuata maagizo ya jinsi ya kutua, hatimaye alitua salama huku maofisa wa kukabiliana na hali ya dharura pamoja na familia yake wakimsubiri.

Loading...

Toa comment