The House of Favourite Newspapers

RUGE KUAGWA VIWANJA VYA GYMKANA BUKOBA

Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti na baadhi ya wanakamati wa maandalizi ya mazishi ya Ruge Mutahaba mkoani Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amesema mwili wa Ruge Mutahaba utaagwa katika Viwanja vya Gyhmkana ndani ya Manispaa ya Bukoba Kabla ya kupelekwa Kabale Halmashauri ya Wilaya Bukoba, kwa ajili ya Ibada na Mazishi.

Gaguti amesema wameamua hivyo kutokana na wingi wa watu wanaotegemewa kuwapo na sehemu ya nyumbani kwa familia ua marehemu kuwa finyu.

Aidha kwa upande mwingine, Gaguti amewaomba wananchi kujitokeza kuulaki mwili wa Marehemu Ruge popote pale utakapopita kwa ajili ya kutoa salaam za mwisho ikiwa ni ishara ya kumuenzi na kumuaga Mzalendo na mwanaharakati wa kweli Marehemu Ruge Mutahaba.

   

Comments are closed.