The House of Favourite Newspapers

Ruvu Shooting Inautaka Ubingwa Ligi Kuu

0

UONGOZI wa Ruvu Shooting, umebainisha kuwa lengo lao kuu ni kufanikisha timu yao inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2021/22.


Timu hiyo ambayo kabla ya
mechi za jana Jumatatu ilikuwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Januari 20, mwaka huu itacheza dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Akizungumza na Spoti Xtra,
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kuwa jambo la kwanza wanalohitaji msimu huu ni kuchukua ubingwa.

 

“Uongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanafahamu umuhimu wa kufanikisha malengo ya klabu
japo tulipitia changamoto ya
kuondoka kwa wawekezaji na wachezaji tisa, lakini hiyo haitokuwa sababu ya kuifanya
timu isifike hatua tunayohitaji
kwa sababu nafasi hiyo ina fursa kubwa na nyingi zaidi kuliko nafasi zingine zote kwenye msimamo,” alisema Bwire.

Leave A Reply