The House of Favourite Newspapers

Dodoma: Mabasi ya Abiria Kusindikizwa na Polisi

0

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma amesema kuanzia kesho mabasi ya abiria kutoka mkoani humo kwenda mikoa mingine yatakuwa yanasindikizwa na askari wa Usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema gari ya askari itakuwa mbele na mabasi yatafuatia kwa msururu na hayataruhusiwa kuovertake.

Agizo hilo limetolewa kufuatia ajali mbaya na ya kizembe iliyotokea leo eneo la Pandambili wilayani Kongwa ikihusisha basi la Baraka linalosafiri kati ya Dodoma na Mtwara.

Kamanda Lyanga amesema Watakuwa wanaweka Askari kwenye Basi la Kwanza, na Mabasi mengine hayatakiwi kulipita hilo basi la kwanza

Lengo ni kudhibiti ajali zinazotokana na Uzembe. Utaratibu huo pia umeonekana kufanyika kwa mabasi yatokayo Mbeya.

Leave A Reply