The House of Favourite Newspapers

Sababu 4 za Kipigo Yanga SC Hizi Hapa

0

MASHABIKI wa Yanga walikuwa na matumaini makubwa sana na timu yao, lakini Jumapili mambo yalikuwa tofauti baada ya kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Rivers ya Nigeria.

 

Huu ulikuwa mchezo wa kwanza wa Klabu Afrika ambapo Yanga wamerejea kwenye michuano hiyo baaada ya kipindi kirefu.

 

Katika mchezo huo ambao awali mashabiki wa Yanga hawakuwa na wazo la kupoteza, Yanga walijikuta wakianza taratibu sana na kuwapa nafasi Wanigeria hao ambao awali waligoma kuingia vyumbani watawale kwenye Dimba la Mkapa.

 

Yanga walifungwa bao lao mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya mabeki kuzembea baada ya kupigwa kona fupi ambapo ilipigwa krosi na kuwapita mabeki wengi waliokuwa katikati na kumkuta mfungaji.

Hata hivyo, kuna sababu nyingi zilizosababisha kipigo hicho kwa Yanga, lakini nne ni muhimu ni hizi hapa.

 

KUPOTEZA NAFASI:

Yanga ambao walikuwa na wachezaji watatu tu wapya kwenye kikosi cha kwanza walipoteza nafasi nyingi sana za kufunga kutokana na kutokuwa makini.

 

Washambuliaji, Hertier Makambo na Feisal Salum walipoteza nafasi za wazi za kufunga mabao, lakini pia Yanga walipiga kona saba kwenye mchezo huo na hakuna iliyozaa matunda huku Rivers wakipiga moja tu na kufunga bao.

 

SUB:

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi anaonekana kuingia kwenye lawama moja kwa moja kutokana na kumtoa Makambo na nafasi yake kuchukuliwa na Athaman, kwa hali ya kawaida ilikuwa ngumu kwa Nchimbi kuwa mkombozi wa Yanga kwa kuwa kwa kipindi kirefu ameshindwa kuonyesha makali yake.

 

Nchimbi kwa kipindi cha mwaka mmoja amefanikiwa kufunga bao moja, hivyo insigekuwa sawa kwake kuwa mkombozi wa Yanga siku ya Jumapili.

 

Pia kwa hali ya kawaida ilikuwa vyema kwa Nchimbi kuingia lakini siyo kuchukua nafasi ya Yacouba kwa kuwa kocha wa Yanga alitaka ushindi alikuwa anatakiwa kumtoa hata mchezaji wa eneo la ulinzi.

 

Mabadiliko ya kuingia Yusuf Athumani yalionekana kuwa sahihi, lakini alikosa uzoefu. Pia kuingia kwa Saidio Ntibazonkiza akichukua nafasi ya Mauya yalikuwa mabadiliko sahihi lakini yalichelewa.

 

PRESHA KUBWA, PAPARA

Wachezaji wa Yanga walionekana kutotulia sana na kuwa na presha ndiyo maana dakika za mwisho walikuwa wanapiga tu mashuti bila kuangalia wanapiga wapi, lakini pia nyuma waliacha mlango wazi muda mwingi na jamaa wangekuwa makini wangepata mabao mengi zaidi.

 

MASHABIKI;

Sawa Yanga wanaweza kusema kuwa walikosa mashabiki na ndiyo sababu nyingine iliyowanyima ushindi kwa Mkapa. Lakini kwa ujumla, lazima Yanga wafanya kazi sana kama wanataka kuvuka.

PHILLIP NKINI, Dar es Salaam

Leave A Reply