The House of Favourite Newspapers

Sababu za ugumba kwa mwanamke

0

ovariancystdiagram.jpgLeo tutaeleza kitaalam sababu zinazofanya mwanamke asiweze kupata mimba na kuzaa kwani tatizo hili husababisha mgogoro katika ndoa nyingi.

Mwanamke anachangia asilimia 40 katika tatizo la ugumba kwenye ndoa. Sababu za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa  ni historia kama amewahi kuwa kwenye uzazi wa mpango kwa muda mrefu (Length of Contraceptive).

Sababu nyingine ni idadi ya mimba na utoaji mimba (Abortions) kwani wanawake wengi ambao hujikuta wakikosa watoto, huku nyuma wana historia ya kutoa mimba.

Lakini pia magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, na uvimbe katika tumbo la uzazi, mirija na mayai (Myoma, tubal or ovarian masses), husababisha tatizo hili.

Mwanamke anaweza kuwa na ugumba kutokana na kukosa tumbo la uzazi au kuwa na bikira (Imperforated Hymen) au kutokwa na uchafu au maji (Discharge) kwenye njia ya uzazi.

Zipo pia sababu za ugumba kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume hizo ni kushindwa kugundua lini, muda yai la kike linapokuwa limekomaa (Ovulation) na  kutambua kama “Ovulation” imetokea.

Pia wahusika wajiulize, je, mirija ya uzazi iko vizuri kuruhusu mbegu za kiume na yai la kike kukutana ili kutungishwa mimba? Je, wanandoa wako vizuri kimwili na kisaikolojia kwa ajili ya kujiandaa kupata mimba?

TIBA NA USHAURI

Ni vizuri kumuona daktari ili aweze kuwasaidia kutambua lini yai la kike linakuwa limekomaa tayari kwa kutungishwa ili tarehe zinapokaribia basi mnakutana kimwili.

Daktari ukimuona anaweza akachukua vipimo vya damu kuangalia magonjwa ya zinaa, mkojo, vipimo vya shinikizo kubwa la damu, kisukari na joto la mwili.

Mwanamke atapimwa HSG (Hysterosaloingography) kuangalia mirija inayosafirisha mayai kama iko sahihi au imeziba kutokana sababu gani na kadhalika.

Asilimia kati 15 hadi 20 ya wanandoa wenye tatizo la ugumba wanaofanyiwa uchunguzi wa kitaalam hupata uzazi (mimba).

Kwa ushauri, wasiliana na daktari aliye karibu akuelekeze nini cha kufanya.

Leave A Reply