The House of Favourite Newspapers

Sabby Angel: Kwa mauno yangu watakaa tu

0

sabby (2) Mduara, Sabrina Omary ‘Sabby’.

Stori: Imelda mtema

Msanii wa filamu ambaye hivi sasa amejiingiza kwenye Muziki wa Mduara, Sabrina Omary ‘Sabby’ amefunguka kwamba anajiamini linapokuja suala la kukata viuno kiasi kwamba haoni msanii wa kike wa kumfunika.

sabby (3)Sabby ambaye ametoa kibao kinachokwenda kwa jina la Inahusu amesema anajua uwezo wa kuimba anao, ukijumlisha na uwezo wake wa kukata nyonga kana kwamba hana mfupa kiunoni anaamini atatusua kimuziki.

“Mimi najua ninaimba miondoko kama ya Shilole lakini niseme tu kwamba, yeye na wasanii wengine wa kike hakuna wa kunifikia kwa mauno,” alisema Sabby.

Leave A Reply