The House of Favourite Newspapers

Safari ya Coutinho Barcelona

Phillippe Coutinho

KIUNGO mpya wa Barcelona, Phillippe Coutinho, juzi alitam­bulishwa kwenye Dimba la Camp Nou, kama mchezaji mpya wa timu hiyo akitokea Liverpool.

Coutinho alitaka kujiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu lakini klabu yake ikagoma kumuuza na sasa imekubali ku­muachia kwa kitita cha pauni mil­ioni 145.

 

Chini ni hatua kwa hatua juu ya safari yake kuanzia mchezaji huyo anajiandaa kuondoka Liverpool, anapanda ndege, anakula maisha kwenye ndege, anacheki mechi ya Liverpool na mambo mengine mengi:

 

Kuhusu Ronaldinho na Lionel Messi: Coutinho anajibu: “Nilipokuwa kijana nilikuwa namuangalia Ronaldinho akicheza, nilikuwa namuagalia akionyesha uwezo wake, leo namuangalia Messi akifanya vilevile.” o namuangalia Messi akifanya vilevile.”

 

Akiwa na mkewe na mtoto wake.

Maisha na familia: Phillippe Coutinho akiwa na mwanaye Maria, mke wake Aine na mama yake Dona Esmeralda kwenye ndege binafsi wakienda Barcelona.

Coutinho aikana jezi yake:  Alipoulizwa kuhusu jezi namba kumi ambayo amekuwa akipenda kuitumia mara kwa mara, Coutinho alijibu:“Hapana haitawezekana, kuna mtu mmoja muhimu sana ambaye anatumia jezi hiyo Barcelona naye ni Lionel Messi, nitavaa jezi yoyote nitakayopewa bila kulalamika.”

Coutinho bata na mwanaye: Baada ya mambo mengi alikuwa amekaa hotelini na mwanaye Maria wakicheki mechi ya Liverpool na Everton.

Bata uwanja wa ndege: Coutinho akiwa uwanja wa ndege wa Luton akisubiri muda wa ndege kuondoka.

 

Amekwenda kwa ajili ya fedha? Coutinho anajibu: “Sijakwenda Barcelona kwa ajili ya fedha, ni kwa kuwa napenda kucheza Barcelona, kuishi Barcelona na familia inapenda Barcelona.”

Alitumia muda mwingi sana kuwa na familia: Coutinho akicheka kufurahia jambo ndani ya ndege.

 

Hee atarudi Liverpool! “Lakini nitarudi Liverpool kuaga wachezaji wenzangu, viongozi pamoja na watu walionisaidia mimi na familia yangu.”

Bosi aliyekula hela yake… Coutinho akiwa na wakala wake Kia Joorabchian akijiandaa kwenda zake Barcelona.

Duu usingizi ulikata… Niliamka kila mara, nilikuwa nalala na kushtuka, hakika nilikuwa naisubiri sana hii siku.”

 

Kuhusu kuondoka Liverpool… “Nilijitoa kwa asilimia 100, asilimia 100 niliitumikia timu hii, miaka mitano nilifanya kila kitu, naipenda klabu hii lakini ni muda wa maisha mengine.”

Haaa! Haaa! Anawasoma wenzake… Anaangalia vitabu vya historia ya Barcelona, anawaona Lionel Messi, Andres Iniesta, Mascherano, Gerrard Pique na Johan Cruyff. Sasa ni muda wa kuweka historia yake mwenyewe.

Coutinho akishuka kwenye ndege: Coutinho akishuka kwenye ndege baada ya kufika nchini Hispania.

Kumbe hawa walimkumbuka mapema: Mara tu baada ya kushuka kwenye ndege Coutinho alipata simu kutoka kwa David Luiz na Willian wakimtakia kila la kheri.

HATIMAYE MAMBO YAMEISHA, AMETAMBULISHWA.

MAKALA NA: PHILLIP NKINI | CHAMPIONI JUMATANO

Comments are closed.