The House of Favourite Newspapers

Safari ya Mwili wa Dkt Mengi Kuelekea Machame – Video

Mwili wa Aliyekuwa mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi, umewasili salama nyumbani kwake Machame, leo Jumatano, Mei 8, 2019.

Maumivu ya mwiba huyasikia ukikuchoma na wakazi wa Kilimanjaro, mwiba umewachoma, machozi yasiyokauka, vilio vya uchungu, maumivu moyoni ndiyo vinavyoonekana sasa hivi. Baba yetu Reginald Mengi, ameenda.

Simanzi na majonzi vimetawala kwenye mioyo ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro waliojitokeza barabarani kuulaki mwili wa marehemu, Dkt. Reginald Mengi.

 

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiligusa gari lililobeba mwili wa Dk Reginald Mengi wakati likitoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kuelekea nyumbani kwao Machame mkoani humo. Mamia ya wananchi wamejitokeza barabarani kutoa heshima za mwisho.

 

 

 

Walizoea kumpokea Shujaa wa Machame, Reginald Mengi kwa furaha na tabasamu lisiloisha hamu lakini leo wanampokea kwa vilio visivyo isha kwani shujaa kaenda, tabasamu halipo, furaha imeenda huzuni imetawala nani wa kushika mkono wanyonge na wenye uhutaji. 

 

 

 

 

Wakazi wa Kilimanjaro wanalia kwani Baba, amelala usingizi mzito.

MOSHI WAMEGOMA – “MSHUSHENI MENGI TUMBEBE WENYEWE”

MWILI wa MENGI Unakaribia NYUMBANI Kwao MACHAME

Comments are closed.