Saido Aiomba Shoo ya Simba Jumamosi Kwa Mkapa

KIUNGOmshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ amesema kuwa anatamani kuanza katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba huku akiweka wazi kuwa matarajio yake ni kuipa ushindi timu hiyo katika mchezo huo muhimu.


Yanga inatarajiwa kumenyana
na Simba katika mchezo wa ligi kuu unatorajiwa kufanyika Desemba 11, mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote kwani kama Yanga itashinda basi itaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 5 huku endapo Simba ikashinda basi itajihakikishia nafasi yakuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 1.


Akizungumza na
Championi Jumatano, Saido alisema kuwa anatamani kuona anapata nafasi ya kuanza katika mchezo dhidi ya Simba ili aweze kuisaidia timu kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ambao ni
muhimu kwao.


“Natamani kuona naisaidia
timu, natamani kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza lakini mamlaka hayo ni ya mwalimu siku zote, hivyo siwezi kumpangia lakini mwenyewe natamani kuona napata nafasi ya kucheza, naamini nitakuwa na mchango mzuri kwa timu.


“Unajua licha ya kuwa tutapata
pointi 3 kama ilivyokuwa michezo mingine lakini kuzipata pointi 3 mbele ya mpinzani wako ni jambo jema, hivyo mengine ambayo yanahusu mchezo wenyewe nadhani waalimu na benchi la ufundi ndio wanahusika zaidi,” alisema kiungo huyo.

Stori: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam


Toa comment