The House of Favourite Newspapers

Sakata la CAG, Wabunge Upinzani Waandaa Mkakati ‘Kumng’oa’ Spika – VIDEO

WABUNGE wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wametishia kupeleka hoja, ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge Job Ndugai baada ya uamuzi wake kuwahamisha baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

 

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, kwa niaba ya wabunge wenzake Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema hatua ya kuvunjwa kwa kamati hizo kuna lenga  kutokaa pamoja na Mkaguzi wa hesabu za serikali bungeni.

 

John Mnyika amesema uamuzi wa kutangaza kuwa hawawezi kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad hawaukubali kuwa hauna tija kwa Taifa.

 

“Kwanza ni kwa nini asisubiri kwanza CAG aitwe na Kamati ya Maadili ahojiwe juu ya kauli yake ndipo ajue cha kumfanya, lakini yeye ameamua kwenda mbali zaidi na kuzuia kufanya kazi na taasisi nzima ambayo ni jicho la Bunge na Watanzania,” amesema Mnyika.

Comments are closed.