The House of Favourite Newspapers

SAKATA LA MTOTO, FLORA AMJIBU MBASHA

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili ambaye pia alikuwa mke wa mwimbaji wa muziki huo, Emmanuel Mbasha, Madam Flora amefunguka kuhusu kitendo cha aliyekuwa mumewe huyo kumlalamikia kupitia mitandaoni kuwa amemnyima fursa ya kumuona japo mtoto wake wa kike waliozaa pamoja wakiwa wanandoa.

 

Flora Mbasha amesema hawezi kulizungumzia jambo hilo kwenye media ama mitandaoni, kwani Mbasha anaujua ukweli.

 

 

“Siwezi kulizungumzia jambo hilo kwenye vyombo vya habari, kama aliandika kwenye instagram nami jibu ningelitolea instagram, ukweli hamuujui sisi ndio tunaujua, kama mahakama iliamua hivyo yeye kuandika instagram kana kwamba mahakama iko instagram, acha aandike, lakini siwezi kuliweka wazi”, amesema Flora.

 

Wawili hao walitalikiana baada ya kesi aliyokuwa akituhumiwa Emmanuel kuisha na kukutwa hana hatia, na kisha Flora kuolewa na kufunga ndoa na Daudi Kusekwa.

Comments are closed.