The House of Favourite Newspapers

Sakata la Polepole, Gwajima, Silaa Latua kwa Majaliwa

0

KAMATI ya wabunge wa CCM imekabidhi ripoti ya mahojiano ya wabunge watatu kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo wawili wanatuhumiwa kwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

 

Wabunge hao ni Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) wanatuhumiwa kwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima Bunge na Humphrey Polepole ambaye anatuhumiwa kwa kushabikia mtandaoni.

 

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Septemba 9, 2021, Katibu wa Wabunge wa CCM, Rashid Shangazi amesema ripoti hiyo imekabidhiwa leo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

 

“Tumeikabidhi leo asubuhi kwa waziri mkuu (Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM naye ataichambua,” amesema.

 

Tayari Bunge limewasimamisha wabunge hao wawili Silaa na Gwajima kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge huku pia Silaa akiondolewa kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP). Kamati hiyo inaweza kutoa uamuzi wa mwisho ama ikapeleka kwenye chama kwa hatua zaidi.

 

Leave A Reply